Taarifa ya utekelezaji wa mkukuta
Download
1 / 27

TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MKUKUTA - PowerPoint PPT Presentation


 • 145 Views
 • Uploaded on

TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MKUKUTA. Mkutano wa Mwaka wa Majadiliano ya Sera za Kupunguza Umaskini na Matumizi ya Rasilimali za Umma, 19 – 21 Novemba, 2008, Dar Es Salaam. DONDOO. Usuli Utangulizi Mafanikio Changamoto Masuala ya Mjadala. 1.0. USULI.

loader
I am the owner, or an agent authorized to act on behalf of the owner, of the copyrighted work described.
capcha
Download Presentation

PowerPoint Slideshow about 'TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MKUKUTA' - zenda


An Image/Link below is provided (as is) to download presentation

Download Policy: Content on the Website is provided to you AS IS for your information and personal use and may not be sold / licensed / shared on other websites without getting consent from its author.While downloading, if for some reason you are not able to download a presentation, the publisher may have deleted the file from their server.


- - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - E N D - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - -
Presentation Transcript
Taarifa ya utekelezaji wa mkukuta

TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MKUKUTA

Mkutano wa Mwaka wa Majadiliano ya Sera za Kupunguza Umaskini na Matumizi ya Rasilimali za Umma, 19 – 21 Novemba, 2008, Dar Es Salaam.


Dondoo
DONDOO

 • Usuli

 • Utangulizi

 • Mafanikio

 • Changamoto

 • Masuala ya Mjadala


1 0 usuli
1.0. USULI

 • MKUKUTA unatekelezwa kupitia michakato ya serikali, Programme za mageuzi/maboresho na programu za maendeleo za kisekta

 • Hatua zinazochukuliwa na asasi zisizo za kiserikali (Sekta binafsi, mashirika ya hiari, vyama vya wafanyakazi, taasisi za kidini)

 • Hivyo, Taarifa ya Utekelezaji wa MKUKUTA imeandaliwa kutokana na taarifa za utekelezaji za wadau hawa.


2 0 utangulizi
2.0. UTANGULIZI

 • Taarifa ya Utekelezaji wa MKUKUTA (2007/8) inatoa sura ya jumla ya mafanikio, changamoto, mambo tuliyojifunza na hatua zinazofuata katika kutekeleza nguzo zote tatu za MKUKUTA

 • Hatua zilizofikiwa katika

  • Ugharimiaji, ufuatiliaji na tathmini

  • Michakato na mageuzi na jinsi hatua hizi zilivyochangia kufikiwa kwa matokeo ya MKUKUTA

 • Taarifa hii imezingatia uwepo wa Taarifa za Utekelezaji za MDAs na za wadau wasio wa kiserikali


Inaendelea
…Inaendelea

 • Taarifa hizi zinatoa hatua zilizochukuliwa na mafanikio kwa kina zaidi

 • Kwa maeneo fulani takwimu hazijabadilika sana ikilinganishwa na taarifa ya 2006/7

 • Aidha katika baadhi ya maeneo takwimu za karibuni hazikupatikana hasa zile zinazotokana na savei.

 • Taarifa hii imejikita zaidi katika kipindi cha hadi Juni 2008

 • Lengo kuu la Ripoti hii ni kutoa taarifa ya hatua zilizofikiwa na kuamsha majadiliano kwa ajili ya kuboresha hatua zinazofuata.


3 0 mafanikio ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini wa kipato
3.0. MAFANIKIO: Ukuaji wa Uchumi na Kupunguza Umaskini wa Kipato

 • Serikali imeendelea kutekeleza sera, mikakati na mageuzi kwa lengo la kuimarisha uchumi

 • Viashiria vingi vinaonyesha mwelekeo mzuri

  • Mfumuko wa bei umepungua kutoka asilimia 7.3 (2006) hadi 7.0 (2007) ingawa ni juu ya lengo la MKUKUTA la asilimia 5

  • Makusanyo ya kodi kama asilimia ya pato la taifa yameongezeka

  • Mikopo kwa sekta binafsi imeongezeka katika mwaka 2007/8

  • Deni la taifa limeongezeka lakini endelevu

  • Thamani ya uwekezaji kutoka nje imeongezeka

  • Ajira mpya 437,205 zimepatikana

  • Pato la taifa limeongezeka na hivyo pato la wastani la mwananchi


2 2 ubora wa maisha na ustawi wa jamii
2.2. Ubora wa Maisha na Ustawi wa Jamii Kipato

 • Hatua mbalimbali zimeendelea kuchukuliwa ili kuboresha maisha na ustawi wa jamii

 • Elimu – utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Elimu umeendelea kutoa mafanikio mazuri

 • Elimu ya Awali

  • Idadi ya watoto walioandikishwa (Net) imeongezeka kutoka asilimia 33.1 hadi 36.2 Gross kutoka asilimia35.2 hadi38.1 mwaka 2008

  • Idadi ya watoto wenye ulemavu walioandikishwa imeongezeka kutoka 685 hadi 2146


Inaendelea1
…Inaendelea Kipato

 • Elimu ya Msingi

  • Watoto walioandikishwa darasa la kwanza (Net) imefikia asilimia 97.2

  • Wanafunzi wanaojiunga na elimu ya sekondari imefikia asilimia 56.7

  • Watoto yatima walioandikishwa wameongezeka kutoka 748,641 (2007) hadi 915,234 (2008)

  • Watoto wenye ulemavu walioandikishwa wameongezeka kutoka 24,003 (2007) hadi 34,661(2008)


Inaendelea2
…Inaendelea Kipato

 • Elimu ya Sekondari

  • Wanafunzi wanaoingia sekondari (NER) imefikia asilimia 23.5. Lengo la MKUKUTA ni asilimia 25 kufikia mwaka 2010

 • Elimu ya Juu

  • Idadi ya wanafunzi wanaojiunga na vyuo vya elimu ya juu wamefikia 75,346 (wasichana ni asilimia 35)


Inaendelea3
…Inaendelea Kipato

 • Afya

 • Programu mbalimbali zimeendelea kutekelezwa katika sekta ya Afya chini ya Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM)

  • Elimu ya kinga

  • Kampeni za chanjo

  • Kuzuia maambukizo

 • Pamekuwa na mafanikio kadha katika eneo la afya ya mtoto na mama

  • Watoto waliochanjwa wakati wa kuzaliwa wamefikia asilimia 73

  • Wagonjwa wa malaria wameendelea kupungua na hivyo kupelekea kupungua kwa vifo vya watoto chini ya miaka mitano

  • Hata hivyo kumekuwa na tofauti ya matokeo haya kati ya mijini na vijijini

  • Chanjo ya surua imefikia asilimia 85

  • Vifo vya kinamama bado viko juu (hakuna takwimu mpya)


Inaendelea4
…Inaendelea Kipato

 • VVU/UKIMWI

 • Juhudi zimeendelea kufanyika kupambana na UKIMWI chini ya Tume ya UKIMWI na Programu ya kudhibiti UKIMWI (NACP)

  • Usimamizi wa mambukizo yanayotokana na zinaa

  • Kupima na ushauri nasaha wa UKIMWI

  • Kuzuia maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto

   • Asilimia 47 ya mama wajawazito walipata huduma ya kupima UKIMWI kwenye vituo vya PMTCT kufikia Desemba 2007

   • Asilimia 34 ya wliopatikana na VVU walipatiwa dawa ya ARV kuzuia maambukizi kwa mtoto


Inaendelea5
…Inaendelea Kipato

 • Sekta ya Maji

 • Serikali imeendelea kutekeleza mipango mbalimbali chini ya Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji

  • Maji vijijini

  • Maji mijini

  • Maji taka

 • Kumekuwepo na ongezeko dogo ya idadi ya watu wanaopata maji safi na salama vijijini

  • Takwimu za savei zinaonyesha kuwa pamekuwa na kupungua kwa asilimia ya wanaopata maji safi na salama

  • Hali ni mbaya zaidi kwa upande wa jiji la Dar Es Salaam


Inaendelea6
…Inaendelea Kipato

 • Kinga ya Jamii

  • Serikali inakamilisha mwongozo wa kinga ya jamii kwa ajili ya kuyashughulikia makundi yaliyo katika hatari ya kuathirika zaidi na umaskini

  • Katika mwaka 2007/8 serikali imeendelea kusaidia makundi yenye mahitaji maalum

   • Serikali imeendelea kuhudumia makazi 17 ya wazee

   • Imeendelea kuhudumia vyuo vitatu vya mafunzo (Vocational training colleges) kwa ajili ya watu wenye ulemavu

   • Serikali imesaidia mafunzo ya stadi watoto yatima 270 walio katika vituo vya kuwalelea (Remands and rehabilitation centres)


2 3 governance and accountability
2.3. Governance and Accountability Kipato

 • Serikali imeendelea kutekeleza Mwongozo wa Utawala Bora

 • Maeneo muhimu ya mwongozo ni pamoja na

  • Ushiriki wa wananchi katika maamuzi yahusuyo maendeleo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi

  • Sekta binafsi na mwongozo wa udhibiti

  • Katiba, utawala wa sheria, usimamizi wa haki na kinga ya haki za binadamu


Inaendelea7
…Inaendelea Kipato

 • Usawa wa jinsia

 • Uwajibikaji, uwazi na uadilifu katika usimamizi wa masuala umma

 • Demokrasia ya uchaguzi na

 • Utumishi wa umma


Inaendelea8
…Inaendelea Kipato

 • Hatua za kuridhisha zimefikiwa katika utekelezaji wa mwongozo

  • Serikali imepitia sheria 12 katika kipindi cha 2007/08

  • Miswada 34 iliandaliwa ambapo miswada 23 ilipitishwa kuwa sheria

  • Serikali pia ilianzisha tovuti kwa ajili ya kupokea maoni/malalamiko ya wananchi


Inaendelea9
…Inaendelea Kipato

 • Serikali imeendelea kutekeleza utaratibu wa kupeleka madaraka zaidi kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa (D by D) ili kuwa na utoaji bora wa huduma kwa umma

  • Wizara 14 zilitathminiwa ili kuona jinsi zinavyotekeleza na kuboresha utaratibu huu

  • Mchakato huu umeboresha matumizi ya fedha zilizopokelewa na LGAs

  • Mchakato pia umeongeza uwazi katika kutenga fedha na usahihi wa fedha zilizotegwa kwa shughuli mbalimbali


Inaendelea10
…Inaendelea Kipato

 • Vita dhidi ya rushwa iliendelea katika mwaka 2007/8

  • Tuhuma 2,887 zilichunguzwa ambapo uchunguzi wa tuhuma 1009 ulikamilika

  • Kesi … zimefikishwa mahakamani katika mwaka 2007/8

 • Serikali imeendelea kuchukua hatua za kuboresha utumishi wa umma

  • Mapitio ya sera ya malipo ya muda wa kati

  • Kuajiri watumishi wapya 36,331 kutoka vyuo vikuu


Inaendelea11
…Inaendelea Kipato

 • Hatua pia zimeendelea kuchukuliwa kuimarisha uwezo mahakama

  • Kuongeza bajeti ya sekta

  • Ongezeko la Majaji wa Mahakama kuu na Mahakama ya Rufaa

 • Juhudi za kuhakikisha haki za binadamu zinalindwa zimeendelea kuimarishwa

  • Kuongezwa kwa uwezo wa mabweni ya wafungwa magerezani

  • Kuboresha usafiri wa watuhumiwa wakati wa kesi zao


2 4 ugharimiaji wa mkukuta
2.4. Ugharimiaji wa MKUKUTA Kipato

 • MKUKUTA unatekelezwa na wadau wote, hivyo na ugharimiaji wake

 • Serikali imekuwa ikitekeleza MKUKUTA kupitia bajeti yake kila mwaka

 • Mwongozo wa Mipango na Bajeti umeendelea kuhimiza utengwaji wa fedha kwa kuzingatia vipaumbele vya MKUKUTA

 • Katika mwaka 2007/8 asilimia 62.7 ya bajeti ilielekezwa kwenye vipaumbele vya MKUKUTA

  • Asilimia 49.37 (Nguzo ya I)

  • Asilimia 29.48 (Nguzo ya II)

  • Asilimia 21.15 (Nguzo ya II)


2 5 ufuatiliaji na tathmini
2.5. UFUATILIAJI NA TATHMINI Kipato

 • Shughuli za ufuatiliaji na tathmini ya MKUKUTA imeendelea kutekelezwa kupitia Mfumo wa Ufuatiliaji wa MKUKUTA, Mifumo ya Ufuatiliaji wa MDAs na ule Mamlaka za Serikali za Mitaa

 • Mfumo wa kitaasisi wa Ufuatiliaji (Kamati na Vikundi kazi) vimeendelea kutekeleza mipango yao ya kazi za ufuatiliaji wa MKUKUTA


Inaendelea12
…Inaendelea Kipato

 • Katika mwaka 2007/8 Mfumo umetoa taarifa mbalimbali

  • Ripoti ya Umaskini na Maendeleo ya Watu – 2007

  • Ripoti ya Tathmini ya Utoaji Huduma Nchini

  • Taarifa ya Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA

  • Kijarida cha MKUKUTA (Electronic)

  • Ushauri wa kisera

 • Aidha tafiti na savei mbalimbali zilifanyika

  • Mapato na Matumizi ya Kaya 2007


3 0 changamoto
3.0. CHANGAMOTO Kipato

 • Changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa nguzo ya I

  • Kupanda kwa bei za petroli

  • Kutokuwa na nishati ya umeme yenye uhakika

  • Uwezo mdogo wa kutumia fedha za matengenezo ya barabara

  • Masuala ya manunuzi katika eneo la barabara (Procurement capacity, timing, planning etc)

  • Kutokuwa na utaratibu wa mikopo ya muda mrefu katika kilimo


Inaendelea13
…Inaendelea Kipato

 • Changamoto katika utekelezaji wa ubora wa maisha na ustawi wa jamii zinahusiana na

  • Masuala ya ubora wa huduma

  • Upatikanaji na gharama za huduma

  • Masuala ya rasilimali watu (Waalimu na Wauguzi)

  • Ongezeko la watu hasa makundi maalum (watoto yatima, watu wenye ulemavu, wazee)

  • Masuala ya manunuzi

  • Rasilimali fedha


Inaendelea14
…Inaendelea Kipato

 • Baadhi ya changamoto katika utawala bora na uwajibikaji ni pamoja na

  • Usimamizi na uratibu wa mageuzi hasa katika kupeleka majukumu kwenye Halmashauri na kupeleka wataalam

  • Kujenga uwezo wa halmashauri kumudu majukumu yanayohamishiwa

  • Utaratibu wa manunuzi unakwamisha


4 0 masuala ya mjadala
4.0. MASUALA YA MJADALA Kipato

 • Haya ni baadhi ya masuala yanayohitaji kupata maelezo sahihi ili kuchukua hatua zitakazosaidia kurebisha au kuongeza kasi

 • Lengo ni kuwezesha kuanzisha mijadala katika michakato ya kisera na mipango iliyopo ili kuboresha hatua zinazochukuliwa

 • Baadhi ya masuala ni pamoja na

  • Ukuaji endelevu wa uchumi na kupungua kwa umaskini

  • Kilimo cha kisasa na kupunguza umaskini


Inaendelea15
…Inaendelea Kipato

 • Nishati

  • Nishati mbadala

  • Nishati ya mimea na uhakika wa chakula

 • Elimu na Mkakati wa Kukuza Uchumi

 • Masuala ya idadi ya watu