slide1 l.
Download
Skip this Video
Loading SlideShow in 5 Seconds..
Ufahamu wa ulimwengu uliokuzunguka! PowerPoint Presentation
Download Presentation
Ufahamu wa ulimwengu uliokuzunguka!

Loading in 2 Seconds...

play fullscreen
1 / 30

Ufahamu wa ulimwengu uliokuzunguka! - PowerPoint PPT Presentation


  • 527 Views
  • Uploaded on

UCHAMBUZI WA VIUMBE Ufahamu wa ulimwengu uliokuzunguka! www.bionet-intl.org | bionet@bionet-intl.org Mchanganuo huu umekusanywa na BioNET (Posa Skelton & Kornelia Rassmann) kwa ushirikiano na wafwatao UTANGULIZI Henrik Enghoff Natural History Museum of Denmark

loader
I am the owner, or an agent authorized to act on behalf of the owner, of the copyrighted work described.
capcha
Download Presentation

Ufahamu wa ulimwengu uliokuzunguka!


An Image/Link below is provided (as is) to download presentation

Download Policy: Content on the Website is provided to you AS IS for your information and personal use and may not be sold / licensed / shared on other websites without getting consent from its author.While downloading, if for some reason you are not able to download a presentation, the publisher may have deleted the file from their server.


- - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - E N D - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - -
Presentation Transcript
slide1
UCHAMBUZI

WA VIUMBE

Ufahamu wa ulimwengu uliokuzunguka!

www.bionet-intl.org | bionet@bionet-intl.org

Mchanganuo huu umekusanywa na BioNET (Posa Skelton & Kornelia Rassmann) kwa ushirikiano na wafwatao

UTANGULIZI

Henrik EnghoffNatural History Museum of Denmark

Ulf GärdenforsArtDatabanken, Swedish Species Information Centre

Fabian HaasAfrican Insect Science for Food

and Health

Chris LyalNatural History Museum, London

Yves SamynRoyal Belgian Institute of Natural Sciences

Ensifera ensifera (Boissonneau, 1840)Mchoraji: Ernst Haeckel

Kiswahili: Melckzedeck K. M. Osore,

Western Indian Ocean Marine Science Association (WIOMSA)

slide2
MIMI NI

NANI?

UTANGULIZI

Je, unatakakujua? Muulizemchambuziwaviumbe

Au bonyeza Kiunganishi hiki …

© Stuart Wynne

slide3

Neno Taxonomy asili yake ni maneno mawili ya kigiriki:

Taxis = mgao/mpangilio, nomos = Sheria

Kugundua

Kutoa jina

Kueleza

Kuainisha

UCHAMBUZI WA VIUMBE NI …Sayansi ya

viumbe

UCHAMBUZI WA VIUMBE NI

Ili kuelewa bioanuai (na mengine yanayohusu…)

slide4
KUGUNDUA

Ugunduzi wa viumbe wapya ndio hatua ya kwanza ya uchambuzi wa viumbe. Kila mwaka viumbe wapya wanagunduliwa kote ulimwenguni, kadri wachambuzi wanapo tembelea maeneo mapya, au vinapopatikana vitendea kazi vipya vya kuchambua sampuli

UCHAMBUZI WA VIUMBE NI

Samaki aina ya Dracula (Dracula fish)

Danionella draculaAmegunduliwa nchini Burma Ameelezewa 2009

© Ralf Britz | Natural History Museum, London

slide5

KUTOA JINA

Electrolux addisoni (Compagno & Heemstra, 2007)

Jina lina muundo gani?

Jina la kisayansi ni hati inayo tambulisha viumbe wote

UCHAMBUZI WA VIUMBE NI

Photo: Phil Heemstra | Wikimedia Commons

Sio fagio lako la kawaida!

kuelezea
KUELEZEA

Sehemu ya mchakato huu inahusu kulinganisha viumbe wanao husiana karibu ili kuthibitisha kama kiumbe fulani ni wa aina mpya.

UCHAMBUZI WA VIUMBE NI

Hypsiboas calcaratus (Troschel, 1848) | Photo: P. J. R. Kok

uainishaji
UAINISHAJI

Jina langu ni Dolly!

Kingdom - Animalia

Phylum - Chordata

Class - Mammalia

Infraclass - Eutheria

Order - Artiodactyla

Family - Bovidae

Subfamily - Caprinae

Genus - Ovis

Species - Ovis aries

UCHAMBUZI WA VIUMBE NI

uainishaji ni muhimu katika maisha yako ya kila siku
UAINISHAJIni muhimu katika maisha yako ya kila siku

Uainishaji ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku.

Hutuwezesha kupanga vitu katika utaratibu unaofaa kama uhakiki mali katika (Supermarket) maduka makubwa.

Je, unategemea kuzipata bidhaa za maziwa zimeorodheshwa pembeni mwa zile za usafi wa nyumbani?

MAJINA NI MUHIMU

Photo: G. R. South

majina ni muhimu katika maisha yako ya kila siku
MAJINAni muhimu katika maisha yako ya kila siku

?

Drawing: Peter Aertsen

Photo: Sergio Kaminski | Wikimedia commons

MAJINA NI MUHIMU

Hebu fikiria kama yasingekuwepo majina ya watu na vitu…

Photo: Wikimedia commons | public domain

majina yanahitajika kwa mawasiliano
MAJINAyanahitajika kwa mawasiliano

Panya

Muis

Ratón

  • Majina ya kawaida au ya lugha za asili ni muhimu kwa mawasiliano ya kila siku lakini matumizi yake ni finyu kutegemea mahali na lugha

マウス

فأس

Ποντίκι

MAJINA NI MUHIMU

Souris

Мышь

Mouse

Mus

Maus

老鼠

© Kornelia Rassmann

majina ya kisayansi kwa mawasiliano kimataifa
MAJINA YA KISAYANSIkwa mawasiliano kimataifa

Alternanthera philoxeroides

Bursaphelenchus xylophilus

MAJINA NI MUHIMU

Photo: L.D. DwinellUSDA Forest Service, United States | forestryimages.org

Photo: Gary BuckinghamUSDA Agricultural Research Service, United States | forestryimages.org

Pseudophilotes sinaicus

  • Kutumia jina la kisayansi ni hakikisho kwamba tunazungumza kuhusu kiumbe fulani bila pingamizi kutokana na eneo letu kijiografia au lugha

Photo: BioNET-NAFRINET

kulijua jina sahihi kunaokoa fedha
KulijuaJINA SAHIHI- kunaokoa fedha

MAJINA NI MUHIMU

Photo: Oliver Spalt | Wikimedia commons

Scotinophara luridaPhoto: Natasha Wright, Florida Department of Agriculture and Consumer Services, Bugwood.org

  • Elimu ya uchambuzi imesaidia kubaini aina ya kombamwiko weusi 24 tofauti inchini Ufilipino, na kati ya hao ni 2 pekee ndiyo waharibifu walioshambulia mchele. Ujuzi huu anaokoa mamilioni ya dola katika matumizi ya viuwa tilifu vya wadudu kwa kuwadhibiti na husaidia kulinda mazingira.
  • See case study no. 39
kutojua jina kunaweza kuua
KUTOJUA JINA- kunaweza kuua!

MAJINA NI MUHIMU

Boletus aurantiacus | Photo: Wikimedia commons | public domain

Nile au nisile? Muulizemchambuziwauyoga (mycologist)!

linnaeus
LINNAEUS

"Ikiwa hauyajui majina ya vitu, ni kazi bure kuelewa umuhimu wa vitu hivyo"

Critica Botanica 1737

MAJINA NI MUHIMU

Carl von Linné(au Linnaeus), ndiye “babawauchambuziwaviumbe”, yeyendiyealiyewekamsingiwamfumowakisasawamajina – wakuwapaviumbemajinakisayansi.

Carl von Linné, 1707-1778 Drawing: AMNH Library

Linnaeus ndiye alieanzisha uainishaji thabiti na sahihi unaohitajika kuieleza bioanuwai, bidhaa za biashara, ununuzi wa mbegu za ukulima, udhibiti wa wadudu waharibifu, au ushughulikiaji wa aina nyingine ya maeneo mengi yanayohitaji ujuzi wa uchambuzi wa viumbe.

umuhimu na uhusiano na bioanuwai
UMUHIMU NA UHUSIANO NABIOANUWAI

© A. De Kesel

Uelewa wa uchambuzi wa viumbe una manufaa kwa sekta nyingi zinazoshirikiana kufanya kazi moja kwa moja au kwa namna mbalimbali na bioanuwai. Ikiwa unajihusisha na biashara ya kuigiza na kutoa bidhaa inchini, uhakiki wa chakula, madawa, afya ya jamii, mabadiliko ya tabia inchi, usalama wa viumbe, kilimo, kilimo cha bustani, uvuvi, sayansi ya mifugo, madini, utalii, au hata kazi za jikoni, masuala ya sekta hizi zote yanahitaji elimu ya dunia hai.

UCHAMBUZI - MANUFAA

Uelewa wa uchambuzi wa viumbe unatuwezesha kuelewa uanuwai wetu wa viumbe.

ufahamu wa dunia hai
UFAHAMU WA DUNIA HAI

© Kornelia Rassmann

Utofauti wa viumbe mbali mbali unafanya dunia yetu iwe ya utata.

Uelewa wauchambuzi wa viumbeunasaidia kufahamu huu utofauti kwa njia ya kupanga na kwa kuuweka ulimwengu wetu katika makundi yanayo eleweka vizuri.

UCHAMBUZI - MANUFAA

uchambuzi wa viumbe manufaa kwa ustawi wa binadamu
UCHAMBUZI WA VIUMBEmanufaa kwa ustawi wa binadamu

Huleta uelewa wa msingi katika maeneo mbali mabli ya manufaa kwa mwanadamu yakiwemo uhifadhi wa bioanuwai, kukabiliana na madadiliko ya tabia nchi, usalama wa viumbe , ukulima,ufugaji samaki, afya, utalii, biashara na mengine mengi.

UCHAMBUZI - MANUFAA

Photo: Bigstockphoto.com

Photo: ???

Photo: Posa A. Skelton

uchambuzi wa viumbe ni swala muhimu kimataifa
UCHAMBUZI WA VIUMBE ni Swala muhimu kimataifa

Husaidia katika maamuzi mema ya sera na udhibiti, hutoa muongozo katika huduma za msingi (kwa mfano katika ukulima, dawa) na ni msingi wa miundombinu ya Malengo ya Milennia yanayohusu kupunguza umaskini, kupambana na magonjwa na kuendeleza mazingira.

UCHAMBUZI - MANUFAA

© Kornelia Rassmann

msingi wa elimu kwa sayansi nyingine
MSINGI WA ELIMU kwa sayansi nyingine

Elimu ya uchambuzi wa viumbe husaidia maeneo mbalimbali ya kisayansi pamoja na sayansi ya hifadhi, biolojia ya uzinduzi, biologia ya uvumbuzi, ikolojia, biojiografia, dawa na mengine mengi.

UCHAMBUZI - MANUFAA

Photo: G. R. South

Photo: BioNET-MESOAMERINET

uhifadhi wa bioanuwai
Uhifadhi wa BIOANUWAI

Kwa kutambua bioanuwai zetu tunaweza kuzihifadhi na kuzitumia kwa uendelevu.

Kwa mfano:

Hifadhi mbalimbali zimeanzishwa kwa sababu ya kugundulika kuwa maeneo ya viumbe hadimuni au maeneo hayo kutambulika kuwa makazi ya viumbe waliodhaniwa kuwa wameshatoweka.

UCHAMBUZI - MANUFAA

© Posa A. Skelton

Brachylophus bulabula – aina mpya ya Iguana(aina ya mjusi mkubwa sana) anaye patikana tu katika nchi ya Fiji.

slide21

TABIA NCHI

kukabiliana na mabadiliko

Kusambaa kwa viumbe kutaathiriwa na mabadiliko ya tabia nchi.

Maktaba ya viumbe

huchangia pakubwa kuhifadhi kumbukumbu za kudumu za kihistoria jinsi viumbe wa aina mbali mbali walivyo sambaa, na kutoa fursa nzuri ya kutabiri uwezekano wa viumbe hao kutoweka, kuenea kwa wadudu waharibifu na maambukizi ya magonjwa na kusaidia katika hatua za kukabiliana na mazingira.

UCHAMBUZI - MANUFAA

© Gert Brovad

viumbe wavamizi wadudu waharibifu usimamizi mzuri
VIUMBE WAVAMIZI & WADUDU WAHARIBIFU Usimamizi mzuri

UtumiziwakombamwikowaainayaCyrtobagoussalviniaekudhibitikueneakwagugumajimkubwawaainayaSalviniamolesta.

Viumbe wavamizi huathiri karibu kila aina ya mazingira duniani na ni tishio kubwa kwa bioanuai. Ili kuepukana na hathari hizi, wachambuzi wa viumbe wenye uzoefu na vifaa vya kutosha wanahitajika kutoa taarifa upesi na kutambua haraka aina na vifaa muhimu vinavyohitajika kutumiwa na viongozi na wanajamii.

UCHAMBUZI - MANUFAA

Photo: Katherine Parys, Louisiana State University, United States

  • See case study no. 27
sera maamuzi
SERA / MAAMUZI

Uelewa wa uchambuzi wa viumbe husaidia kuratibu sera na mfumo wa muongozo.

Kwa mfano:

Mkataba kwa ajili ya Biashara ya Kimataifa ya Viumbe Wanaotishia

Kuangamia (CITES ), hutegemea taarifa sahihi za uchambuzi kufanikisha udhibiti mzuri wa biashara ya aina ya viumbe hao, kama vile orchids (aina ya mmea wa maua).

Viumbe wanaoorodheshwa na Mkataba kwa ajili ya Biashara ya Kimataifa ya Viumbe Wanaotishia Kuangamia (ujulikanao kama CITES) hulindwa kwa viwango na aina tofauti dhidi ya matumizi holela.

UCHAMBUZI - MANUFAA

Karibu aina zote za mimea hii zimeorodheshwa na CITES, idadi kubwa katika Kiambatanisho cha pili (appendix II) ambacho kinajumuisha aina ambazo sasa hazitishiwi na kuangamia lakini zinaweza kuan-gamia kama biashara haitadhibitiwa kwa makini.

© Martin Voggenreiterclockwise: Ophrys fusca, Orchis italica, Cypripedium calceolus, Ophrys lutea

ugunduzi wa viumbe hai afya
UGUNDUZI WA VIUMBE HAI & AFYA

© Posa Skelton - Morinda citrifolia

© Stuart Wynne - Niphates digitalis

Mimea yenye dawa ni muhimu katika sehemu nyingi duniani, na uchambuzi wa viumbe hutumika kutambua mimea yenye manufaa, kama vile tunda la Noni.

UCHAMBUZI - MANUFAA

Sifongo wa baharini (marine sponges) ni chanzo kizuri cha misombo ya muhimu kwa kutengeneza madawa, viungo vya chakula na vifaa vingine kwa matumizi ya kibiashara. Elimu ya uchambuzi wa viumbe husaidia kugundua na kubainisha haya.

slide25

For a similar case study see case study no. 8

UHAKIKA WA VIUMBE HAI & BIASHARA

Mdudu asiye fahamika anapopatikana katika shehena ya kilimo, anaweza kusababisha kupungua kwa kasi ya biashara duniani na shehena husika inaweza kucheleweshwa kwa muda mrefu na gharama kubwa ikisubiri mdudu huyo atambuliwe barabara. Katika hali hii, uelewa wa uchambuzi wa viumbe unaweza kuokoa fedha.

UCHAMBUZI - MANUFAA

Madai ya kuwepo kwa aina fulani ya mba (anaye julikana kama Karnal bunt fungus) katika shehena ya ngano toka nchi ya Australia kulisababisha kukataliwa kwa shehena hiyo kuingia nchini Pakistan. Kwa kutumia uchambuzi wa viumbe, ilibainika kwamba chembechembe zilikua sio za mba husika ambao hutambulika kwa kuvamia maeneo. Kutatuliwa kwa swala hilo kulizuia kusitishwa kwa biashara ya ngano yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni nne.

Tilletia indica|Photo: Ruben Durán, Washington State University, Bugwood.org

kupunguza umaskini uhakika wa chakula
KUPUNGUZA UMASKINI&UHAKIKA WA CHAKULA

Kupunguza umaskini, uhakika wa chakula na uhifadhi wa viumbe hai huenda sambamba. Kimataifa, umaskini na uhaba wa chakula mara nyingi hupatikana sehemu zilizopoteza idadi kubwa ya viumbe hai.

Uelewa wa uchambuzi wa viumbe husaidia kuendeleza mazingira yenye afya katika nchi zinazoendelea, ambapo hupatikana kiwango kikubwa cha bioanuai duniani, lakini pia idadi kubwa ya watu wa kipato cha chini vijijini wakitishiwa na upungufu wa bioanuai.

UCHAMBUZI - MANUFAA

© bluerain | Dreamstime.de

© imagedirekt.de

uchambuzi wa viumbe kuendeleza elimu yetu
UCHAMBUZI WA VIUMBE:kuendeleza elimu yetu

Hadi sasa, aina takriban milioni 1.8 wamegundu-liwa. Inakisiwa yakwamba idadi kamili ni kati ya milioni 5 hadi 50.

Tafakari mfano huu:

Katika utafiti uliyohusisha kiumbe aitwaye cricket (anayefana kama panzi) wa nchini Australia, asilimia 76 ya viumbe hao waligundu-liwa kuwa wapya.

From Otte, D., and R. D. Alexander. 1983. The Australian Crickets (Orthoptera: Gryllidae). Academy of Natural Sciences of Philadelphia.

Viumbe wapatao 18,500

wa aina impya waligunduliwa mwaka 2007

CHANGAMOTO

Unka boreena (Otte & Alexander) | Photo: David Rentz

slide28
UKUBWA tu wa KUKUMBATIWA

Sio hoja

Uchambuzi unahusu sio tu viumbe wenye karama wanaojulikana na kila mtu, kama vile Nyangumi, na wanyama wengine wakubwa wanaoishi nje ya Afrika kama Giant Panda, na Polar bear (aina ya dubu).

CHANGAMOTO

© Tatiana Goydenko | Dreamstime.com

Unahusu pia viumbe wadogo wanaosababisha mazingira yetu kustawi. Baadhi ya viumbe hawa wadogo wadogo wanaweza kutufaa maishani mwetu (mfano chachu) ama kutuathiri (mfano mbu anaye eneza malaria)!

© Josef Szasz–Fabian | Dreamstime.com

slide29
DUNIA ina SHANGAZA

Hippocampus satomiae | © Rudie Kuiter

© John Sear

Sayari yetu ina maajabu mengi ya kushangaza na hazina nyingi – viumbe wapya hugunduliwa kila siku lakini mwanadamu (Homo sapiens kwa jina la kisayansi) haupi ugunduzi huu thamani inavyostahili.

Kiumbe huyu aitwaye Seahorse (mwenye umbile la farasi mdogo sana anayeishi baharini) aliyegunduliwa rasmi mwaka 2008 ndiye mnyama mdogo sana wa aina yake. Ana urefu wa 13.8 mm na kimo chake ni takriban 11.5mm.

CHANGAMOTO

una hamu ya kujua mengi kuhusu uchambuzi wa viumbe
Una hamu ya kujua mengi kuhusuUCHAMBUZI WA VIUMBE?

Hapa utapata maelezo zaidi kuhusu...

Uchambuzi wa viumbe

Global Taxonomy Initiative (GTI, UN Convention of Biological Diversity)|

European Distributed Institute of Taxonomy (EDIT) |Natural History Museum, London, UK) |Royal Belgian Institute of Natural Sciences | BioNET-International

Aina ya viumbe

Encyclopedia of Life (EoL) |Wikispecies | ARKive |IUCN Red List |Top 10 New Species Discoveries International Institute for Species Exploration (IIES) | Tree of Life | Census of Marine Life (CoML) | Catalogue of Life (ITIS, Species2000) | Global Biodiversity Information Facility (GBIF)

Umuhimu wa uchambuzi, aina ya viumbe & bioanuai BioNET case studies |GTI case study on taxonomy & climate change |

UN Convention of Biodiversity – 2010 International Year of Biodiversity

MAELEZO

Photos: BioNET-SAFRINET, BioNET ANDINONET, BioNET-EAFRINET, BioNET-NAFRINET