650 likes | 1.57k Views
YALIYOMO. MPANGO MKAKATI MUUNDO UONGOZI. MAANA YA MPANGO MKAKATI (STRATEGIC PLANNING. Mpango ni mfumo wa kimaandishi unaoonesha kazi zinazotakiwa kufanywa na hatua mbalimbali za kufikia malengo yaliyowekwa kwa muda maalumu. UMUHIMU WA KUWA NA MPANGO MKAKATI.
E N D
YALIYOMO MPANGO MKAKATI MUUNDO UONGOZI
MAANA YA MPANGO MKAKATI (STRATEGIC PLANNING • Mpango ni mfumo wa kimaandishi unaoonesha kazi zinazotakiwa kufanywa na hatua mbalimbali za kufikia malengo yaliyowekwa kwa muda maalumu.
UMUHIMU WA KUWA NA MPANGO MKAKATI • Mara nyingi ufanisi wa utekelezaji huwa mzuri • Inaweka mpangilio mzuri wa matumizi ya rasilimali. • Inasaidia kuratibu kazi zote ili kufikia lengo. • Inasaidia kuweka vipaumbele • Inasaidia kutoendeshwa na matakwa ya wafadhili
MPANGO MKAKATI • Maana ya mpango mkakati • Umuhimu wa kuwa na mpango mkakati • Hatua za kuwa na mpango mkakati
UMUHIMU WA KUWA NA MPANGO MKAKATI • Inatoa mwelekeo wa jumuiya na kuonyesha njia • Inaonyesha shughuli / kazi kuu za jumuiya • Inasaidia kujua nyenzo zinazohitajika na hivyo kuchukua jitihada ya kuzitafuta • Inasaidia kutathimini kama lengo la jumuiya limefanikiwa au halikufanikiwa kwa muda uliopangwa . • Inasaidia katika ugawaji wa majukumu na dhamana miongoni mwa wanachama.
HATUA ZA KUTAYARISHA MPANGO MKAKATI • Matayarisho (preparation) • Uhakiki wa mission, vision na value • Historia asasi ( organization bio- line ) • Uchambuzi wa mazingira ( environment scan) • Malengo makhususi ( specific objectives) • Kazi au shughuli • Viashirio ( indicators) • Matumaini na mashaka assumption and risk. • Ufuatiliaji na tathimini ( monitoring and evaluation)
MATAYARISHO /MAANDALIZI YA MPANGO MKAKATI • Wakati wa kuandaa au kutayarisha zoezi la mpango mkakati ni muhimu kuzingatia mambo yafuatayo. • Sababu ya kutayarisha mpango huo • Nani watashiriki katika zoezi hilo • Je washiriki wamealifiwa na kukubali • Je washiriki wanaelewa sababu ya kuandaa mpango mkakati huo • Nani ataongoza zoezi la mpango mkakati • Ni yepi maandalizi na mahitaji muhimu kwa ajili ya kufanikisha zoezi hilo.
MIFANO YA VISION…… • Progressive and civil society which citizens, their association and institutions of society enjoys equitable access and control over the benefit of human development .(NGORC) • Capable society that uses education to bring its development (The ELITE).
MIFANO YA MISSION…. • Changamoto encourages self – employment through provision of credits, quality education and according to the needs of Zanzibar society.( changamoto) • NGORC enhance the competency and credibility of CBOs, grass root CSOs, build capacity of young men and women and to catalyze the emergence of an enabling environment for civil society thus enabling it to contribute effectively to social development in zanzibar and some selected arears in East Africa
UHAKIKI WA VISION, MISION NA MAADILI • Vision: ni ile picha au ndoto ya kimaendeleo ambayo asasi inatarajia kuifikia • Ni yale mabadiliko chanya ya kimaendeleo ambayo asasi inataka walengwa wayafikie na kufaidika nayo MFANO WA VISION • Children and youth friendly society ( ZACA) • Inclusive and equitable society mobilized for sustainable development in Ole . ( ODC) • Poverty free society (CHANGAMOTO)
MISSION • Ni kazi kuu ambazo asasi inajikita ili kufikia vision yake. • Maswali muhimu ya kujiuliza katika kuandika mission ya asasi ni, sisi ni nani , tutafanya nini na vipi, tunafanya kwa nani na wapi. MIFANO YA MISSION ZACA contributes in the improvement of most vainarable children’s condition and promotion of positive behaviour change of youth in Zanzibar though advocacy , training , provision of psycho-social support and education . (ZACA)
VALUES • Ni imani au maadili ambayo asasi imejiwekea, inayathamini na kuyazingatia katika utendaji wake wa kila siku, mahusiano miongoni mwa wana asasi, walengwa na hata jamii kwa ujumla, MFANO WA VALUE ZA ASASI.
HISTORIA YA ASASI ( ORGANIZATION BIO- LINE) • Hapa unaeleza kwa ufupi mambo yafuatayo: • Sisi ni nani • Jina la asasi • Eleza iwapo ni NGO, CBO, VDO n.k • Imeanza lini • Kama imesajiliwa • Idadi ya wanachama , wanaume wangapi? Wanawake wangapi? • Inafanya kazi gani na wapi?
UCHAMBUZI WA KIMAZINGIRA ENVIRONMENTAL SCAN) • Uchambuzi wa kimazingira unatusaidia kujua fursa na vikwazo ( opportunity and threats vilivyomo katika mazingira yaliyotuzunguka • Mambo unayoyaangalia katika uchambuzi huu ni pamoja na • Kukubalika kwa jamii, walengwa • Kukubalika kuhitajika kwa huduma zenu • Serikali na mipango yake, serikali ina mipango • Gani katika nyanja ambayo mnafanyia kazi • Wafadhili • Asasi nyingine : ushirikiano /ushindani.
MALENGO MAHSUSI ( SPECIFIC OBJECTIVES) • Baada ya kufanya uchambuzi wa kimazingira na kujua fursa ya vikwazo vilivyopo tunajiwekea malengo makhususi • Malengo mahsusi ni yale mambo hasa tunayodhamiria kuyafanyia kazi na kuona matokeo yake baada ya muda tuliojipangia Mifano ya malengo makhsusi • mashirikiano yanakuwepo na kuimarika baina ya serikali, asasi za kiraia na sekta ya biashara katika kuleta maendeleo
HISTORIA YA… • Malengo yetu makuu ni yepi? • Mafanikio makuu tuliyoyapata tokea kuanzishwa kwa asasi • Matatizo tuliyokumbana nayo ambayo yamesababisha kutofanikiwa kwa utekeleaji wa malengo.
UCHAMBUZI WA KIMAZINGIRA • Hali ya kisera:sera ya serikali inaathiri vipi mipango yenu. • Hali ya kisheria: sheria inaathiri vipi mipango yenu. • Hali ya siasa • Geografia • Utamaduni
MIFANO YA MAL… • Taasisi za kiraia ziwe zimeimarika kitaaluma na kiuwezo ili ziweze kutimiza malengo zilizojipangia na hivyo kuchangia katika maendeleo ya kijamii. • Wanajamii wapate taarifa muhimu na sahii za kimaendeleo ili nao washiriki kikamilifu katika mchakato wa maendeleo • Vijana wawe wanashiriki katika uongozi wa nyanja mbalimbali na mchakato wa maendeleo
KAZI /SHUGHULI (ACTIVITIES) • Vipi tutaweza kufikia malengo mahususi tuliyojiwekea • Kwa kila lengo mahususi tuliyojiwekea tunatakiwa tuainishe kazi tutakazofanya ambazo zitatuwezesha kufikia malengo yetu • Kwa mujibu wa malengo yaliyoainishwa hapo juu kazi zinaweza kuwa pamoja na • Kujenga uwezo wa asasi kwa njia mbalimbali
VIASHIRIO (INDICATORS ) • Tunatakiwa kuweka bayana kabisa viashirio ambavyo vitatusaidia kupima mafanikio wakati na baada ya utekelezaji wa kazi • Swali la msingi hapa ni kujiuliza ni vipi tutajua iwapo lengo tulilojiwekea limefanikiwa ama la. • Hivyo kwa kila lengo mahsusi na kazi tulizoainisha tunatakiwa tuweke viashirio ili kupima mafanikio yake.
VIASHIRIO • Mabadiliko mbalimbali ya sera yaliyofanywa • Kuongezeka kwa mchango wa sekta ya biashara kwaw miradi ya maendeleo ya kijamii.
KAZI… • Kufanya tafiti na kutoa machapisho • Kufanya uchambuzi wa sera mbalimbali za kitaifa ili kuona ufanisi na athari zake kwa asasi za kiraia na jamii kwa ujumla
MIFANO YA VIASHIRIA • Kwa mujibu wa malengo mahsusi na kazi tulizoziainisha hapo juu, viashiria vinaweza kuwa pamoja na • Idadi ya asasi za kiraia zilizojengewa uwezo • Kukua kwa ushiriki wa vijana katika uongozi • Vituo vya habari za maendeleo vilivyoanzishwa • Idadi ya waandishi wanaofika katika vituo vya taarifa za maendeleo kwa lengo la kupata taarifa mbali mbali za maendeleo
MATUMAINI/DHANA NA MASHAKA(RISK & ASSUMPTION) • Mambo mazingira au hali fulani tunayoitumiania ili kazi tulizojipangia ziweze kufanyika kwa ufanisi . • Kuvurugika kwa hali hiyo kunavyoweza kuvuruga kazi na malengo yetu • Ni matumaini yetu hali ya utulivu wa kisiasa itaendelea ikitokea kuvurugika kwa hali ya utulivu mipango yetu inaweza kuvurugika
UFUATILIAJI NA TATHIMINIMONITORING & EVALUATION • Eleza kwa ufupi mipango ya asasi katika kusimamia na kutathimini mwenendo wa kazi ili kuweza kupima mafanikio • Mbinu gani utatumia • Dhana utakazotumia • Kila baada ya muda gani • Nani watakaohusika na zoezi hilo n.k
MAANA YA MUUNDO • Muundo ni mfumo unaoonesha vyeo vya watu mbalimbali ndani ya jumuiya au ni mtiririko maalumu wa nafasi mbalimbali za uongozi katika jumuiya ambao una lengo la kuwa na ufanisi katika utekelezaji wa kazi
SIFA ZA MUUNDO MZURI • Muundo wa asasi ukidhi haja • Muundo uwe na uwezo wa kubadilika kulingana na wakati na hali halisi • Muundo wa asasi unatakiwa ueleweke kwa wanachama wote • Muundo wa jumuiya lazima uwe sawa na ule uliyomo kwenye katiba zao.
MUUNDO • Maana ya muundo • Umuhimu wa muundo • Sifa za muundo mzuri
UMUHIMU WA MUUNDO • Kunakuwa na urahisi na ufanisi wa utendaji kazi • Kila mtu anajua kazi yake • Unarahisisha mahusiano ya jumuiya • Mipango ya kazi hutekelezwa kwa urahisi zaidi • Unasaidia wanachama na viongozi wapya kujifunza na kuelewa shughuli za jumuiya kwa urahisi zaidi, • Jumuiya inakuwa haiyumbishwi na watu wa nje.
MAANA YA UONGOZI • Uongozi ni uwezo wa kuwaelekeza na kuwahamasisha watu wengine katika jumuiya (kamati) ili kufikia lengo lililokusudiwa
UONGOZI • MAANA YA UONGOZI • SIFA ZA KIONGOZI MZURI • AINA ZA UONGOZI
SIFA ZA UONGOZI • Awe na uwezo mzuri wa kumbukumbu • Awe na ushirikiano mwema ndani na nje ya jumuiya • Awe anaongoza kutokana na mazingira yaliyopo • Awe mtumishi wa watua • Awe mwenye kujiamini na kuwaamini wenzake • Anapofanya kosa akili na awe tayari kujirekebisha • Awe mmbunifu • Awe mtu mwenye kuthamini michango ya wengine Aweze kuwashajilisha wanachama wenzake Awe na uwezo wa kuwaunganisha wanachama
SIFA ZA KIONGOZI MZURI … • Awe mbunifu • Awe mtu mwenyekuthamini michango ya wengine • Aweze kuwasajisha wanachama wenzake • Awe na uwezo wa kuchambua mambo na kuwa na upeo • Aongoze kulingana na kanuni za jumuiya • Awe muwazi • Awe na uwezo wa kupatanisha • Asiwe na jazba • …………………(ziko nyingi
SIFA ZA KIONGOZI MZURI • Awe na uwezo wa kutekeleza malengo ya jumuiya • Awe na uwezo wa kusimamia kazi • Awe muadilifu kwa wanachama • Awe hawabagui wanachama kwa misingi ya dini • Awe anatenda haki • Awe anachukua jukumu la kubeba dhamana. • Aweze kuwajibika kwa wanachama wake • Awe shupavu katika kutetea maslahi ya jumuiya
SIFA ZA KIONGOZI MZURI • Awe na uwezo mzuri wa kumbukumbu • Awe na ushirikiano mwema ndani na nje ya jumuiya • Awe anaongoza kutokana na mazingira yaliyopo • Awe mtumishi wa watu • Awe mwenye kujiamini na kuwaamini wenzake • Anapofanya kosa akiri na akubali kujirekebisha
AINA ZA UONGOZI • Ungozi wa kiimla ( kidikteta) • Uongozi wa kiholela ( Havinimbi) • Uongozi wa kidemokrasia
UONGOZI WA KIIMLA • Unatumia amri • Unapenda kujilabu ( kujigamba/kuwa na imani ndogo kwa wanachama • Amri zinatoka juu kuja chini • Kiongozi anawagawa wanachama • Wakati mwingi maslahi ya wanachama hayapewi uzito • Hauko wazi juu ya mapato na matumizi • Hauruhusu kukosolewa
UNGOZI WA KIDEMOKRASIA • Unakuwa na uamuzi wa pamoja • Wanachama wanatakiwa ushauri • Sababu za kutoa maamuzi zinatolewa • Maoni ,mawazo na michango ya wanachama inakaribishwa, kusikilizwa na kuzingatiwa • Kuna hali ya kukosoana na kupongezana • Kuna uwajibikaji miongoni mwa wanachama na uongozi
UONGOZI WA KIHOLELA • Kiongozi hana mamlaka, kila mtu anafanya anavyotaka • Maamuzi yanatolewa na yeyote yule • Ufanisi huwa mdogo kwa kukosekana usimamizi • Hamu ya kazi inapungua • Umoja na shahuku huwa duni • Kila mtu anamlaumu mwenzake • Ubadhirifu wa rasilimali huwa mkubwa • Unazalisha majungu na vikundi visivyoleta maslahi ya jumuiya • Unadhoofisha uhai wa jumuiya
UONGOZI WA KIDEMOKRASIA • Ufanisi unakuwa mzuri • Uhai wa asasi una imarika • Kunakuwa na tija na ubunifu • Rasilimali zinatumika kwa ufanisi • Kunakuwa na ukweli na uwazi • Kuna hisia ya dhamana