1 / 36

UJASIRIAMALI

UJASIRIAMALI. NI NANI MJASIRIAMALI?. Mjasiliamali ni mtu anaekuwa na maono ya biashara,anayegundua fursa,akakusanya rasilimali na kuthubutu kuanzisha mradi kwa imani kwamba atafanikiwa katika mradi huo Ni mtu anaebadilisha mawazo kuwa bidhaa au biashara. UMUHIMU WA UJASIRIAMASLI.

matana
Download Presentation

UJASIRIAMALI

An Image/Link below is provided (as is) to download presentation Download Policy: Content on the Website is provided to you AS IS for your information and personal use and may not be sold / licensed / shared on other websites without getting consent from its author. Content is provided to you AS IS for your information and personal use only. Download presentation by click this link. While downloading, if for some reason you are not able to download a presentation, the publisher may have deleted the file from their server. During download, if you can't get a presentation, the file might be deleted by the publisher.

E N D

Presentation Transcript


  1. UJASIRIAMALI

  2. NI NANI MJASIRIAMALI?

  3. Mjasiliamali ni mtu anaekuwa na maono ya biashara,anayegundua fursa,akakusanya rasilimali na kuthubutu kuanzisha mradi kwa imani kwamba atafanikiwa katika mradi huo • Ni mtu anaebadilisha mawazo kuwa bidhaa au biashara

  4. UMUHIMU WA UJASIRIAMASLI • Kuongeza ajira • Kukuza uchumi wa nchi • Kuongezeka kwa mawazo mapya ya biashara

  5. NINI SIFA ZA MJASILIAMALI?

  6. Anatafuta fursa • Mbunifu • Anayediriki kutenda • Anayejiamini • Anayetafuta habari • Anatimiza makubaliano katika kazi • Asiyeyumba • Anautashi wa ubora na ufanisi • Anayeweka malengo • Anayepanga na kusimamia

  7. ANAETAFUTA FURSA • Hufanya vitu kabla ya kuambiwa au kulazimishwa na matukio. • Hujitahidi kupanua biashara, bidhaa au huduma katika maeneo mengine. • Huchukua fursa zisizo za kawaida kuanzisha biashara mpya, kupata ufadhili, vifaa, ardhi, mahali pa kazi au msaada.

  8. ANAEKABILINA NA HATARI • Hukokotoa hatari kwa kujua na kutathmini vitu mbadala. • Huchukua hatua za kupunguza hatari au kudhibiti matokeo. • Hujiweka katika mazingira yanayohusu changamoto au hatari za wastani.

  9. MBUNIFU • Anaejitofautisha na wenzake kwa namna tofauti tofauti kama rangi ya bidhaa,muundo,namna ya kuuza,kifungahio n.k

  10. ANAEHITAJI UFANISI NA UBORA • Hutafuta njia za kufanya mambo vizuri, kwa haraka sana na kwa gharama nafuu. • Hufanya mambo ambayo yanafikia au kuzidi viwango vya ubora. • Huweka au kutumia taratibu ili kuhakikisha kuwa kazi inakamilika kwa wakati au kuwa kazi inafikia viwango vya ubora vilivyokubaliwa.

  11. ANAEJIAMINI NA KUJITAWALA • Hushikilia uamuzi wake wakati wa kukabiliana na upinzani au kukosa mafanikio mapema. • Huonyesha kujiamini katika uwezo binafsi wa kukamilisha kazi ngumu au kukabiliana na changamoto.

  12. ANAETEKELEZA MKATABA AU MAKUBALIANO • Hujitolea binafsi au kutumia jitihada zisizo za kawaida kukamilisha kazi. • Hushirikiana na wafanyakazi au kuwafuatilia kuhimiza kazi ifanyike. • Hujitahidi kuwaridhisha wateja na kuwa na uhusiano mzuri wa muda mrefu katika kipindi kidogo tena.

  13. ANAETAFUTA TAARIFA • Hutafuta mwenyewe taarifa kutoka kwa wateja, wasambazaji au washindani. • Hufanya utafiti binafsi wa jinsi ya kutoa bidhaa au huduma. • Hushauriana na wataalamu kuhusu ushauri wa kibiashara au kitaalamu

  14. ANAEPANGA MALENGO • Hupanga malengo na shabaha ambavyo vina umuhimu na kuleta changamoto binafsi. • Hufafanua kwa uwazi malengo mahsusi ya muda mrefu. • Huweka malengo ya muda mfupi yanayopimika.

  15. ANAESHAWISHI NA KUWASILIANA • Hutumia mikakati ya makusudi ili kushawishi wengine. • Huwatumia watu muhimu kama mawakala kukamilisha malengo yake. • Hufanya kazi ya kuanzisha na kudumisha mawasiliano ya kibiashara

  16. TOFAUTI KATI YA MJASIRIAMALI NA MFANYABIASHRA • Hufnya vitu kwa kuiga • Huajiri mfanyakazi ili biashara ifanye vizuri na kupata faida kubwa • Anafanya kazi kwa haraka haraka na wakati mwingine hapati anachokitarajia • Mara nying hufanya vitu kwa ubunifu • Huajiri mtu na kumpatia ujuzi ili aweze kuihudumia jamii vizuri • Anafanya shughuli kwa taratibu ili aweze kupata matokeo anayoyahitaji

  17. TOAUTI………………. • Anaangalia mafanikio kwa maendeleo yake mwenyewe au kwa wafanyakazi wake au kwa mbia mwenzake • Anajitahidi sana kuwashinda washindani wake • Mjasiriamali anaangalia mafanikio kwa atakachokiacha • Anajishindanisha mwenyewe

  18. TOFAUTI………….. • Anamuona mteja kama chanzo cha mauzo na mapato • Anaogopa sana kuchukua maamuzi ambayo yanaweza kuhatarisha faida yake • Yeye ndio yeye,asipokuwepo mambo yanakwama • Anamuona mteja kama chanzo cha kazi yake • Anachukua maamuzi wakati mwingine ni hatari kwa kazi yake • Huweka mikakati ya shughuli kuendelea hata kama yeye hatakuwepo

  19. TOFAUTI……….. • Lengo ni kupata faida • Mara nyingi hutumia njia za mkato katika kutatua matatizo au ugumu wa jambao • Lengo ni kubadilisha dunia • Panapokuwa na ugumu hufuata njia sahihi ya kutatua

  20. JE UKO TAYARI KUWA MJASIRIAMALI? TAFADHALI ANGALIA MASWALI YAFUATAYO NA KISHA UJIPIME MWENYEWE KITU CHA MSINGI NI KUWA MUAMINIFU WAKATI UNAJIPIMA

  21. Je unaanzavitumwenyewe? 1.Ninafanya vitu mwenyewe. Hakuna anayepaswa kuniambia nifanye jambo. 2.Kama mtu akiniwezesha kuanza, ninaendelea vizuri. 3.Sitaraji jitihada zozote mwenyewe mpaka nilazimike kufanya hivyo..

  22. Unaonajekuhusuwatuwengine? 1.Ninapenda watu. Ninaweza kuelewana na mtu yeyote. 2.Nina marafiki wengi - Simhitaji mwingine zaidi. 3.Watu wengi wananiudhi.

  23. Unawezakuongozawengine? 1.Watu wengi hunifuatisha na huendelea kwa mafanikio ninapoanzisha kitu. 2.Ninaweza kutoa maagizo kama mtu ananifahamisha tunachopaswa kufanya. 3.Ninamwachia mwingine aendeleze kazi. Kisha ninaendelea kama ninataka.

  24. Unawezakushikamadaraka? 1.Ninapenda kusimamia mambo na kuhakikisha yanakamilika. 2.Ninaweza kushika madaraka kama nikilazimika, bali ningependelea mtu mwingine ashike. 3.Kila wakati yupo mtu anayetaka kujionyesha jinsi alivyo stadi wa vitu. Ninasema mwacheni afanye hivyo.

  25. Wewenimpangajiwamipangomzuri? 1.Ninapenda kuwa na mpango kabla ya kuanza jambo. Kwa kawaida mimi ndiye hupanga mambo wakati kundi linataka kufanya kitu. 2.Ninafanya vizuri labda mambo yavurugike. Kisha huacha. 3.Mambo yanapagwa vizuri kisha kitu kinajitokeza na kusababisha matatizo mengi mno. Kwa hiyo nayachukulia mambo kama yanavyokuja.

  26. Wewenimfanyakazimzuri? 1.Ninaweza kuendelea madhali ninapenda. Sijali kuendelea kufanya kazi kwa bidii kwa jambo ambalo ninalitaka. 2.Nitafanya kazi kwa bidii kwa muda, lakini ninapotosheka, ninaacha. 3.Sioni kwamba kufanya kazi kwa bidii kunawafikisha popote.

  27. Je unawezakutoamaamuzimazuri? 1.Ninaweza kuamua kitu kwa haraka nikipaswa kufanya hivyo. Kwa kawaida huwa SAWA. 2.Ninaweza kama nina muda wa kutosha. 3.Nikilazimika kuamua jambo haraka, baadaye ninafikiri ningeweza kuamua vinginevyo.

  28. Watuwanawezakuaminiunachokisema? 1. Wanaweza. Sizungumzi vitu nisivyokusudia. 2. Najaribu kuwa muwazi wakati wote. Lakini wakati mwingine ninasema tu kilicho rahisi zaidi. 3. Kwa nini ujisumbue kama mtu mwingine haoni tofauti

  29. Unawezakuyashikilia? • Kama nikiamua kufanya jambo. Siruhusu kitu chochote kinizuie. • Kwa kawaida ninakamilisha ninachokianza – kama kinakwenda vizuri. • Kama hakiendi mara moja, ninaacha. Kwa nini kusumbua akili yako?

  30. Afyayakoninzurikiasigani? • Huwa siumwi! • Nina nguvu ya kutosha kwa mambo mengi ninayotaka kufanya. • Huishiwa nguvu haraka kuliko rafiki zangu walio wengi.

  31. MATOKEO YA ZOEZI LA JUU • Kama majibu yako mengi yaliyokuwa ya 1 huenda una kitu kinachofaa katika kuendesha biashara. Kama sio, unaelekea kuwa na matatizo zaidi kuliko ambavyo unaweza kuyashughulikia mwenyewe. Afadhali utafute mwenza ambaye ni mzuri zaidi katika mambo ambayo huyawezi. Kama majibu mengi yalikuwa ya 3, hata mwenza mzuri hataweza kukupatia msaada unaohitaji.

  32. VITU GANI VINAVYOCHANGIA MTU KUWA MJASILIAMALI NCHINI TANZANIA?

  33. Nchini Tanzania,watu wengi wanaingia kwenye shughuli za jiasiriamali na kuanzisha biashara ndogo kwa sababu kuu tatu (3)

  34. Kwanza,kukosa elimu ya kutosha ambayo ingesaidia katika kupata ajira rasmi • Pili,Kukosa njia mbadala ya kupata kipato na hivyo kupelekea ugumu wa maisha katika familia • Tatu,Kurithi kutoka kwa wazazi • Nne,Kutotaka kuajiriwa au kuwa chini ya mtu

  35. HITIMISHO • Kiwango cha ujasiriamali nchini Tanzani bado kipo chini ukilinganisha na nchi nyingi.Hii inatokea wakati tuna rasilimali nyingi sana ikiwemo bahari,maziwa,mbuga za wanyama,ardhi nye rutuba,dhahabu,milima n.k • Changamoto kubwa ipo kwetu na serikali katika kubadilisha rasilimali hizi kwa ufanisi na mafanikio ili ziwe bidhaa au huduma zitakazopelekwa sokoni katika bei ya ushindani

  36. MWISHO KABISA • AHSANTENI SANA • THANK YOU • WABEJA SANA • WAKORA WAITU • MURAKOZE CHANE

More Related