1 / 2

MATUKIO MUHIMU YA TEKNOLOJIA – MAONI YA WANAKEMIA

I. NISHATI NA USAFIRISHAJI.

tamma
Download Presentation

MATUKIO MUHIMU YA TEKNOLOJIA – MAONI YA WANAKEMIA

An Image/Link below is provided (as is) to download presentation Download Policy: Content on the Website is provided to you AS IS for your information and personal use and may not be sold / licensed / shared on other websites without getting consent from its author. Content is provided to you AS IS for your information and personal use only. Download presentation by click this link. While downloading, if for some reason you are not able to download a presentation, the publisher may have deleted the file from their server. During download, if you can't get a presentation, the file might be deleted by the publisher.

E N D

Presentation Transcript


  1. I. NISHATI NA USAFIRISHAJI Wanakemia na wahandisi kemikali wamechangia sana katika masuala ya nishati na usafirishaji ambayo yametupa nguvu za kupanua uwezo wetu zaidi kuanzia ardhini, angani na hadi anga za juu zaidi. Mnamo karne ya 19 watu walikuwa wakitumia kuni au mkaa wa mawe kuongeza joto katika nyumba zao wakati wa baridi, wakitumia vibarati na mishumaa kwa kuonea wakati wa usiku, wakisafiri kwa kutumia reli na boti dhaifu, farasi au miguu. Wakati mahitaji ya nishati yakiongezeka karibu karne mbili zilizopita, kemia imeongeza na kuimarisha vyanzo mbali mbali vya nishati kama kugundulika kwa mafuta, uzumbuzi wa betri pamoja na kukua kwa teknolojia mbali mbali za kuweza kupatikana kwa nishati mbadala. Kuimarika kwa kemia kumechangia mabadiliko makubwa katika sekta ya usafirishaji ikiwemo miundo mbali mbali ya magari, ndege, vyombo vya anga za juu pamoja na barabara. Kufuatia ugunduzi wa metali, madini pamoja na mafuta kutoka katika vyanzo mbali mbali na kugundulika kwa njia tofauti mbadala, kemia imebadili mfumo wetu wa maisha. MATUKIO MUHIMU YA TEKNOLOJIA – MAONI YA WANAKEMIA I.1. Vyanzo vya Nishati (Energy Source) Matumizi ya makaa ya mawe Utafiti na uchimbaji wa petroli Nishati ya Nyuklia Vyanzo mbadala vya nishati I.2. Hifadhi ya Nishati ya Umeme na Vyanzo vya Nishati vinavyohamishika (Electrical Energy Storage and Portable Power Sources) Betri za kawaida (Single-use batteries) Betri za kurudia chaji (Rechargeable batteries) I.3. Vifaa vya kutengenezea Barabara na Madaraja(Materials for Roadways and Bridges) Saruji ya Zege (Concrete) Lami (Asphalt) Metali na alloi (mchanganyo wa metali bora na fifi) (Metals and alloys) Teknolojia ya utunzaji na matengenezo ya vifaa (Maintenance and repair technology) I.4. Mafuta ya jamii za Kemikali za Petroli (Petrochemical Fuels) Upatikanaji wa petroli kutoka katika mafuta yasiyosafishwa Nyongeza zitokanazo na mafuta (Fuel additives) Kichachamshi (Catalytic converters) I.5. Vyombo vya usafiri (Automotive Vehicles) Vifaa vya kisasa kwa usafiri wa raha na salama Vifaa vya plastiki (Plastic components) Teknolojia ya kutengeneza matairi (Tire technology) I.6. Mwendoanga (Aeronautics) Puto kubwa linalojazwa kwa hewa moto (Hot-air balloons) Heliamu (Helium) Mafuta ya roketi (Rocket fuel) Vifaa vya kutengenezea ndege na roketi (Construction materials for aircrafts and rockets)

  2. I. NISHATI NA USAFIRISHAJI Matukio: 1882 Kituo cha kwanza cha umeme utokanao na makaa ya mawe kuanza kusambaza umeme kwa matumizi ya nyumbani. 1884 Mjerumani Gottlieb Daimler atengeneza injini ya kwanza ya gari yenye kutumia mafuta ya petroli, kitoa-moto pamoja na pistoni. 1902 Kingo za barabara zilizotengenezwa kwa lami iliyotokana na mafuta ghafi. 1913 Joto maalumu (thermal cracking) kuvunja molekyuli (molecules) zisizohitajika kwa kutumia moto zatumika ili kupata wingi na ubora wa petroli. 1921 Thomas Midgley, Jr. agundua matumizi ya tetraethyl lead kama kiongezo katika petroli ili iweze kufanya kazi vizuri. 1936Mfaransa Eugene Houdry aboresha matumizi ya petroli kwa kugundua kipimo cha oktani (high-octane) katika mafuta hayo. 1947 Kampuni ya Marekani ya B. F. Goodrich yaanzisha mipira (matairi) isiyotumia mirija. 1949 Eveready Battery Co. yagundua betri za alkaline. 1954 Betri ya kwanza ya silikoni inayotegemea mwangaza wa jua yazinduliwa katika Bell Labs. 1958 Boeing 707 yaanza kazi na kubadilisha mfumo mzima uliozoeleka wa usafiri wa anga. 1970s Mpango wa mafuta yasiyotumia madini ya risasi yazinduliwa, kuondosha madini ya risasi katika petroli. 1975 Kichachamshi chaanzishwa katika magari. 1980-1990s Betri za Lithium-ion zapata umaarufu kwa matumizi ya simu za mikononi (cellular phones) pamoja na laptop. 1981 Columbia Space Shuttle chombo cha kwanza cha anga duniani mabaki yake kuweza kutumika tena. Kituo cha umeme utokanao na makaa ya mawe Gari la Daimler katika stempu Ujenzi wa barabara kwa kutumia lami Thomas Midgley Jr. Eugene Houdry akiwa na mfano wa kichachamshi (catalytic converter) Bango-ujumbe asili la matairi ya Goodrich Betri ya kwanza ya silikoni inayotegemea mwangaza wa jua Boeing 707 Mpango-kazi wa vichachamshaji Mpango-kazi wa betri za lithium-ion Space shuttles

More Related