1 / 28

Neno la Uzima

Neno la Uzima. Februari 2013. Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mautini kuingia uzimani, kwa maana twawapenda ndugu. (1Yh 3:14). Yohane anaandikia jumuia za kikristo alizozianzisha kipindi ambapo zinapitia wakati mgumu.

sera
Download Presentation

Neno la Uzima

An Image/Link below is provided (as is) to download presentation Download Policy: Content on the Website is provided to you AS IS for your information and personal use and may not be sold / licensed / shared on other websites without getting consent from its author. Content is provided to you AS IS for your information and personal use only. Download presentation by click this link. While downloading, if for some reason you are not able to download a presentation, the publisher may have deleted the file from their server. During download, if you can't get a presentation, the file might be deleted by the publisher.

E N D

Presentation Transcript


  1. Neno la Uzima Februari 2013

  2. Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mautini kuingia uzimani, kwa maana twawapenda ndugu. (1Yh 3:14)

  3. Yohane anaandikia jumuia za kikristo alizozianzisha kipindi ambapo zinapitia wakati mgumu.

  4. Mafundisho ya uongo kuhusu imani na maadili yalikuwa yanaanza kuenea, na jamii ya kipagani ambamo wakristo waliishi ilikuwa kati na adui kwa roho ya Injili.

  5. Ili kuwasaidia, mtume anaonyesha njia ya pekee: kumpenda ndugu, kuishi sheria ya upendo waliyoipata tangu mwanzoni ambayo, anaona kama mhutasari wa amri zingine zote.

  6. Kwa kufanya hivyo watajua ‘maisha’ ni nini. Wataongozwa, yaani kwa undani zaidi na zaidi katika ushirika na Mungu na watang’amua Mungu-upendo. Na kwa kuwa na mang’amuzi hayo, watathibitishwa katika imani na kuweza kukabiliana na kila shambulizi, na hasa katika nyakati za hatari.

  7. Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mautini kuingia uzimani, kwa maana twawapenda ndugu. (1Yh 3:14)

  8. Tunajua...’ Mtume anamaanisha ujuzi utokanao na mang’amuzi. Ni kama kusema: ‘tumeng’amua, ‘tumegusa kwa mkono wetu’.

  9. Ni mang’amuzi ambayo wakristo walioinjilishwa na Yohane walifanya tangu mwanzoni mwa uongofu wao. Tunapoweka katika matendo amri za Mungu, kwa namna ya pekee amri ya upendo kwa jirani, tunaingia katika maisha ya Mungu.

  10. Lakini je, wakristo wa leo wanafahamu mang’amuzi haya? Bila shaka wanajua kuwa amri za Mungu zina lengo maalum. Yesu daima anasisitiza kuwa haitoshi kusikiliza Neno la Mungu; sharti kuliishi (taz. Mt. 5:19; 7:21; 7:26).

  11. Baadala yake, kisicho dhahiri zaidi kwa wengi, aidha kwa kuwa hawajui au wana ujuzi wa kinadharia tu bila kuwa na mang’amuzi, ni uzuri wa maisha ya kikristo ambayo mtume anayadhihirisha. Tunapoishi amri ya upendo, Mungu anatuchukua, na ishara isiyokosewa ya hili ni ile amani, ile furaha anayotujalia kuonja tayari hapa duniani.

  12. Hapo kila kitu kinaangazwa, kila kitu kinakuwa katika ulinganifu. Hakuna tena tofauti kati ya imani na maisha. Imani inakuwa ile nguvu inayoingiana na kuunganisha matendo yetu yote.

  13. Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mautini kuingia uzimani, kwa maana twawapenda ndugu. (1Yh 3:14)

  14. Hilo Neno la Uzima linatuambia kuwa upendo kwa jirani ni njia ya kifalme inayotuongoza kwa Mungu

  15. Kwa kuwa sote ni watoto wake, hakuna kilicho cha muhimu kwake zaidi ya upendo kwa jirani yetu. Hatuwezi kumpa furaha kubwa zaidi kuliko tunapompenda jirani yetu.

  16. Na kwa kuwa upendo kwa jirani unaleta ushirika na Mungu, ni chemchemi isiyokauka ya mwanga wa ndani, ni kisima cha maisha, cha matunda ya kiroho, cha upyayusho endelevu.

  17. Ni kinga dhidi ya uozo, ugumu, ulegevu ambavyo vinaweza kujikita kati ya wakristo; kwa neno moja inatutoa katika mauti kuingia uzimani’.

  18. Kinyume chake, upendo ukikosekana, kila kitu kinanyauka na kufa. Tukijua hili tunaelewa kwa nini mitazamo mingine imeenea katika ulimwengu wa sasa: kutokuwa na ari na upeo, udhaifu, kukereka, kutamani kutoroka, mmomonyoko wa maadili, n.k.

  19. Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mautini kuingia uzimani, kwa maana twawapenda ndugu. (1Yh 3:14)

  20. Ndugu ambao mtume anamaanisha, awali ya yote ni wanajamii yetu. Kama ni kweli kuwa tunatakiwa kuwapenda wote, ni kweli pia kuwa upendo wetu unatakiwa kuanzia kwa wale tunaoishi nao, halafu utaenea katika ulimwengu wote.

  21. Tunatakiwa kufikiria kwanza wanafamilia yetu, wafanyakazi wenzetu, wanaparokia yetu, jumuiya yetu au shirika letu la kitawa.

  22. Upendo wetu kwa jirani hautakuwa halisi na wenye muelekeo sahihi kama hautaanzia hapa. Popote tunapojikuta, tunaitwa kujenga familia ya wana wa Mungu.

  23. Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mautini kuingia uzimani, kwa maana twawapenda ndugu. (1Yh 3:14)

  24. Neno hili la Uzima linafungua mtazamo mpana sana.

  25. Linatuhimiza katika safari ya kimungu yenye matokeo yasiyotabirika. Zaidi ya yote linatukumbusha kuwa katika ulimwengu kama wetu, wenye nadharia ya ushindani, ambamo anayeishi ni mwenye nguvu, mjanja, asiye mnyofu, na wakati mwingine kila kitu kinaonekana kama kimekufa ganzi kutokana na tamaa ya kumiliki vitu na ubinafsi, jibu letu linatakiwa kuwa upendo kwa jirani.

  26. Hii ndiyo dawa inayoweza kuuponyesha ulimwengu. Hakika, tunapoishi amri ya upendo, si tu maisha yetu yanatiwa nguvu, bali, kila kitu kinachotuzunguka kinaguswa. Ni kama wimbi la joto la kimungu, linaloenea na kukua, likipenya mahusiano ya mtu mmoja na mwingine, kundi moja na lingine, na kidogo kidogo kubadili jamii.

  27. Kwa hiyo tuamue sasa! Ndugu wa kuwapenda kwa jina la Yesu, tunao sote, na tutakua nao daima. Hebu tuwe waaminifu kwa upendo huu. Hebu tuwasaidie wengine kuwa hivi. Tutaelewa mioyoni mwetu maana ya ushirika na Mungu. Imani itastawi, mashaka yatatoweka, hakutakuwa tena na kukerwa. Maisha yatajaa sana.

  28. Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mautini kuingia uzimani, kwa maana twawapenda ndugu. (1Yh 3:14) “Parola di Vita” inatangazwa na Movement of Focolare. Matini hii Imetolewa katika Città Nuova n. 9/1985Chapa cha Anna Lollo akishirikiana na Fr. Placido D’Omina (Sicily, Italy). Maelezo ya Neno la Uzima inatafsiriwa katika lugha 96 na kilugha na kuwafikia mamilioni ya watu katika dunia nzima kwa njia ya maandishi, radio, TV na kwa njia ya Tovuti. Kwa kupata maelezo www.focolare.org PPS hiyo, katika lugha mbalimbali inatangazwa katika www.santuariosancalogero.it (na hapo unaweza kupakua)

More Related